KWA NINI UCHAGUE ST. THOMAS INSTITUTE OF MANAGEMENT AND TECHNOLOGY (STIMAT)?
Chuo hiki ni moja ya vyuo vichache kabisa katika ukanda wetu chenye Hati-idhini ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika fani saba (7).
Sisi ni chuo kinachotoa mafunzo nyumbufu na yenye ubora kilichopo Songea mjini katika eneo tulivu la Ruhuwiko karibu na kiwanja cha ndege cha Songea.
Eneo hili awali lilikuwa linamilikiwa na vyuo vikuu viwili vya Mt, Joseph yaani kile cha Kilimo na Tehama, hivyo basi lina miundombinu ya kuweza kumudu kiasi kikubwa cha wanafunzi ndani nan je ya chuo.
Jirani na chuo kuna huduma zote muhimu ambazo mwanafunzi anazihitaji aweze kusoma bila shida kama maduka, nyumba za ibada, soko, hospitali na kadhalika.
Songea ni moja ya miji ambayo gharama za Maisha zipo chini na hivyo kuwa chagua la wanafunzi wengi.
Chuo chetu kinatoa mafunzo kwa unyumbufu unaowasaidia hata wale waliopo kazini kwa kuwa na ratiba inayojali walio kazini pia.
Wanafunzi wengi wamekuwa wakihamia na kufurahia taratibu zetu hasa ufuatiliaji mahsusi wa mfumo wa NTA.
Chuo kina kompyuta za kutosha na kuwawezesha wanafunzi kupata mafunzo ya TEHAMA kwa vitendo.
Chuo kina maktaba yenye vitabu Zaidi ya 10,000 vikiwamo vitabu vya kielektroniki.
Wanafunzi wetu hukuzwa na kuthaminiwa kama watu wazima.
Chuo kina walimu wenye sifa na ubora katika Nyanja zote na Zaidi ya 90% ya walimu wetu wamesajiliwa na NACTE kama walimu wa elimu ya Ufundi “technical teachers”
Chuo kinatoa ushauri wa ajira na namna ya kujiunga na elimu ya juu.
STIMAT inaruhusu vyama vya wanafunzi vya dini mbalimbali na klabu za kitaaluma.
STIMAT inatoa mafunzo yenye ubora kwa gharama nafuu.
STIMAT inatoa skolaship za namba mbili kwa wanafunzi walengwa na ina utaratibu wa kutoa nafuu ya ADA kwa wanafunzi waliona ufaulu BORA.
STIMAT inajali sana mafunzo kwa vitendo na wanafunzi wetu hupata nafasi ya kujifunza sehemu za kazi kila semesta.
STIMAT inajali mafanikio na Maisha yako kuliko alama zako darasani.
Na mwisho, STIMAT ipo kukusaidia “Usome Zaidi, Ili Uwe Zaidi” kama ilivyo KauliMbiu ya Chuo chetu.