JINSI YA KUFIKA SONGEA
Songea ipo kusini mwa Tanzania na unaweza kufika ukitokea sehemu mbalimbali za nchi yetu kwa njia kubwa tatu, yaani kupitia Iringa, Lindi au Mbinga. Mabasi maarufu ya Super Feo, Selous, Sajda na New Force huondoka miji mbalimbali kuja Songea. Kila sku alfajiri katikamiji ya dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mtwara, Masasi, Mbeya, Mbinga, Sumbawanga, Njombe na Tunduru kuna mabasi yanayosafiri kuja Songea moja kwa moja ukiacha yae yanayokuja kwa kuunganisha safari zake.
Pia kuna usafiri wa meli kupitia ziwa Nyasa kwa wale wanaotoka pembezoni kwa ziwa hilo au ndege na kutua moja kwa moja Ruhuwiko Songea katika kiwanja cha ndege kinachopo ukingoni mwa chuo chetu.
Nauli za mabasi hupangwa na LATRA (www.latra.go.tz) na ufikapo Songea mjini ni vyema ukashukia kituo cha mjini kuliko stendi kuu iliyopo eneo la Msamala. Iwapo umefika mchana waweza kujachuoni kwa kutumia daladala kwa kiasi cha nauli y ash, 400 tu au bodaboda kwa kiasi cha Shilingi 2000 au 4000 wakati wa usiku. NAuli za mabasi kwa sasa ni kama ifuatavyo:
Iringa (Tsh19,000, masaa 8) and Dar es Salaam (Tsh46,000, masaa 14), Mbeya (Tsh24,000, masaa 8), Njombe (Tsh10,000, masaa 4), Mbamba Bay (Tsh8,000, masaa 5), Tunduru (Tsh10,000, masaa 4) na Masasi (Tsh21,000, masaa 7).